Jumatatu 3 Agosti 2026 - 05:45
Ayatullah Arafi atoa majukumu mapya kwa wasimamizi wa Hawza, wanazuoni na wahubiri

Ayatullah Arafi amesisitiza ulazima wa kuendelea kuwa na utayari wa kila upande kwa wasimamizi wa Hawza, wanazuoni wa dini na wahubiri ili waendelee kutekeleza wajibu wao wa kielimu, kiroho, kimapinduzi na wa kiutendaji wakiwa pamoja na wananchi na vijana, pamoja na kuwa tayari kikamilifu kwa kuanza mwaka mpya wa masomo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Alireza Arafi, kupitia barua aliyowaandikia wasimamizi wa ngazi za makao makuu na wa ngazi za utekelezaji za Hawza, pamoja na wanazuoni wa dini na wahubiri kote Iran na duniani, amewapa jukumu la kuendelea kuwa na utayari wa kina, wa pande zote, mpana na wa mchanganyiko, ili waendelee kutekeleza nafasi yao ya kielimu, kiroho, kimapinduzi na ya kiutendaji sambamba na wananchi, vijana wapendwa na nguvu za Mapinduzi.

Mkurugenzi wa Hawza pia alisisitiza umuhimu wa kuwa tayari kikamilifu kwa ajili ya kuanza mwaka wa masomo, pamoja na kuweka mazingira ya kukuza maendeleo ya kielimu, kiroho na kimapinduzi ya Hawza na wanafunzi wake wapendwa, hususan waliopokelewa hivi karibuni, kwa kuzingatia hali zote.

Majukumu maalumu kwa manaibu na wasimamizi wa Hawza

Ayatullah Arafi pia aliwataka manaibu na wasimamizi wa ngazi za makao makuu na wa ngazi za utekelezaji wa Hawza kubuni programu maalumu za kuanza mwaka wa masomo, vipaumbele vya mwaka ujao, mipango ya mageuzi na programu mbalimbali, huduma mpya kwa wanahawza, pamoja na mikakati ya tablighi, kimapinduzi na ya kiutendaji kwa mwaka ujao wa masomo.

Yafuatayo ni maandishi kamili ya barua ya Mkurugenzi wa Hawza:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu

Manaibu na wasimamizi waheshimiwa wa Makao Makuu na wa Qom,

Wasimamizi waheshimiwa wa mikoa,

Wanazuoni watukufu wa dini na wahubiri wenye heshima kote Iran na duniani.

Assalamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Nawatakia nyote mafanikio zaidi.

Kwa unyenyekevu na kwa dhati kabisa, ninawashukuru kila mmoja wenu wapendwa, pamoja na wenzenu wote waheshimiwa, wanazuoni wote, walimu, wahubiri na wanazuoni wa dini nchini Iran na duniani, pamoja na Hawza, hususan Hawza za Qom, Najaf, Mashhad na Tehran, kwa juhudi zenu za kujitolea, za kimapinduzi, endelevu, za kiutendaji na za kifikra katika kipindi chote cha Vita vya Tatu vya Kulazimishwa, pamoja na shughuli za mazishi na kumbukumbu za Kiongozi Shahidi (Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) na mashahidi wengine watukufu wa Iran na Mhimili wa Muqawama nchini Iran, Iraq na duniani kote.

Pia ninawashukuru kwa shughuli zenu za kishujaa katika mawakibu, viwanjani na katika kuutetea Uislamu, Mapinduzi ya Kiislamu, Mfumo wa Kiislamu, taifa letu pendwa, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi, vikosi vya ulinzi na wananchi wa Iran. Vilevile ninazishukuru taasisi zote tukufu za Hawza, Makao Makuu ya Balagh Mubin katika vituo vya mikoa na miji, Baraza la Uratibu wa Taasisi mbalimbali, mabaraza ya mikoa ya Hawza za Kielimu, pamoja na viongozi, wasimamizi, watumishi, walimu, wahubiri na wanafunzi wa shule na vituo vya Qom na kote nchini, hususan katika mikoa iliyokuwa mstari wa mbele wa vita.

Aidha, ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Mar'ajii Wakuu wa Taqlid na Baraza Kuu la Hawza. Pia ninawashukuru kwa dhati wahubiri wote wapendwa waliotekeleza jukumu lao katika miezi miwili ya Muharram na Safar nchini kote na duniani, pamoja na wote walioshiriki na kutoa mchango wao katika matembezi makubwa ya ustaarabu ya Arubaini na mawakibu ya Arubaini nchini Iran na Iraq. Ninamuomba Mwenyezi Mungu awape wote hao heshima na utukufu, na aupe Uislamu, Mapinduzi ya Kiislamu, Iran na Mhimili wa Muqawama ushindi katika mapambano haya ya kihistoria na ya kiustaarabu. Pia ninatumaini kuwa juhudi zote hizi, huduma na kujitolea huku vitakubaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu na kupata uangalizi wa Imam wa Zama, Al-Hujjah (Mwenyezi Mungu aharakishe faraja yake).

Baada ya ujumbe, taarifa na maelekezo mengi yaliyotolewa, napenda kukumbushia mambo matatu yafuatayo:

1. Kuna ulazima wa kuendelea kudumisha utayari wa kila upande, wa kina, mpana na wa mchanganyiko wa wanazuoni wa dini, Hawza, taasisi za Hawza, shule na vituo vya Hawza kote nchini. Aidha, ni muhimu kuendelea kutekeleza nafasi ya kielimu, kiroho, kimapinduzi na ya kiutendaji sambamba na wananchi, vijana wapendwa na nguvu za Mapinduzi kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa.

2. Ni lazima kuwepo utayari kamili kwa ajili ya kuanza mwaka wa masomo na kuweka mazingira ya kukuza maendeleo ya kielimu, kiroho na kimapinduzi ya Hawza na wanafunzi wapendwa, hususan waliopokelewa hivi karibuni, kwa kuzingatia hali zote za uwanjani na kwa mujibu wa maelekezo yaliyotolewa.

3. Ni lazima manaibu na wasimamizi wote wa ngazi za makao makuu na wa ngazi za utekelezaji waandae na kutangaza kwa ufupi, ifikapo mwisho wa mwezi wa Mordad, programu zao maalumu za kuanza mwaka wa masomo, vipaumbele vyao vya mwaka ujao, mipango yao ya mageuzi, programu na huduma mpya kwa wanahawza, pamoja na mikakati yao ya tablighi, kimapinduzi na ya kiutendaji kwa mwaka ujao wa masomo.

Asanteni Sana

Alireza Arafi

Mkurugenzi wa Hawza Nchini Iram.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha